Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC apiga marufuku matangazo ya msiba

GARI YA MSIBA Magari ya kutangaza Msiba yapigwa marufuku

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua amepiga marufuku magari yanayofanya matangazo ya misiba jijini hapa baada ya kuchukua miili ya watu waliofariki dunia hospitalini, akisema yamekuwa yakileta hataruki kwa wananchi na kujenga hofu.

Amesema hayo leo Jumanne Agosti 10, 2021 huku akiiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya doria na kuwachukulia hatua wamiliki wa magari hayo watakaobainika.

"Kumekuwa na tabia ya familia za watu wanaopoteza maisha kukodi magari ya matangazo na kuanza kutangaza maeneo mbalimbali ya jiji na kutaja majina ya wapendwa wao, sasa kwa niaba ya mkuu wa mkoa nimepiga marufuku rasmi leo Agosti 10 2021,"

"Ikumbukwe agizo hilo la kupiga marufuku hata aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alikataza lakini sasa suala hilo limeibuka kwa kasi ya ajabu na kila baada ya dakika kadhaa unasikia tangazo la msiba, hivyo kusababisha shughuli za kiuchumi kusimama kwa muda."

Dk Chuachua amesema agizo hilo lianze mara moja na ndugu wanaofikwa na msiba, wawasiliane kifamilia kufanya taratibu za mazishi na kuhusu suala la matangazo kutoka hospitali mpaka kwenye maziko marufuku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live