Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC apiga marufuku kuajiri walinzi wasiokuwa na mafunzo ya kijeshi

IMG 20221224 WA0020 DC apiga marufuku kuajiri walinzi wasiokuwa na mafunzo ya kijeshi

Wed, 4 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serimali ya wilaya ya Iringa imezitaka kampuni za Ulinzi kuajiri wafanyakazi waliopitia mafunzo ya kijeshi ili kuboresha ufanisi wa kazi katika sekta ya ulinzi wa mali za UMMA, serikali,watu binafsi na mashirika binafsi.

Akifunga mafunzo ya Jeshi la akiba katika kata ya Masaka mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa kitendo cha makampuni ya ulinzi yaliyopo wilaya ya Iringa kuajiri walinzi wasio na mafunzo kinakinzana na taratibu na sheria zilizopo, huku kikiwanyima fursa askari waliopitia mafunzo ya kijeshi.

Moyo aliliagiza Jeshi la Polisi kuanzisha ukaguzi maalum dhidi Makampuni ya ulinzi Wilayani Iringa ili kujiridhisha endapo walioajiriwa Kwa kazi ya Ulinzi wamekidhi vigezo vinavyotambuliwa kwa mujibu wa sheria.

Alizitaka kampuni za Ulinzi zizopo wilaya ya Iringa kuwaondosha kazini wafanyakazi wasiopitia mafunzo ya Jeshi,Kabla ya Serikali kuchukua hatua ya kuyafutia leseni makampuni hayo.

Kiongozi huyo ameeleza mpango wa Serikali ya wilaya katika kusaidia kundi kubwa la vijana waliohitimu mafunzo hayo..

Moyo alimazia kwa kusema kuwa Serikali haiwezi kuvumilia kuona makampuni hayo yakikiuka sheria kwa makusudi akibainisha kuwa kitendo cha kuajiri watu wasiopitia mafunzo kuwa ni chanzo cha uhalifu katika maeneo mbalimbali

Kwa upande wao wahitibu wa mafunzo haya ya jeshi la akiba katika risala yao wameeleza miongoni mwa changamoto kuu ni kukosa ajira katika makampuni ya ulinzi kwani makampuni yaliyo mengi yanaajiri watu wasiopitia mafunzo ya jeshi

Naye Diwani wa kata ya masaka Methew Nganyagwa akimualika Mgeni wa heshima katika hafla hiyo amesema mafunzo hayo yamekuwa na tuija kubwa ya kimaendeleo katika kata hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live