Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amelalamikia kitendo cha jeshi kuwapiga wananchi kufuatia mgogoro wa eneo la Kijaka-Kimbiji uliodumu kwa muda mrefu sasa.
RC Chalamila alifanya mkutano wa hadhara katika eneo la Kijaka-Kimbiji ambako kuna mgogoro mkubwa kati ya Wananchi na Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mkuu wa Mkoa amewasikiliza wananchi na upande wa jeshi ambapo ameahidi kurudi tena huku akiwataka wananchi kutulia.
"Tutafuatilia nyaraka kama eneo litaonekana ni la jeshi la wananchi Tanzania watapewa na kama eneo litaonekana la wananchi watapatiwa," alisema RC Chalamila.
Katika ziara hiyo, RC Chalamila aliambatana na mkuu wa wilaya hiyo, Halima Bulembo, wataalam kutoka TARURA na TANROAD na wataalam wengine kutoka ofisi yake na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.