Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC amaliza mzozo wakulima Tanzania,Kenya

DCC DC amaliza mzozo wakulima Tanzania,Kenya

Thu, 7 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, amezungumza na viongozi wa Kenya wanaoongoza maeneo yaliyo mpakani mwa Kenya na Tanzania kupitia Mpaka wa Namanga, ili kutatua kadhia inayowakumba Watanzania waliokodisha mashamba katika taifa hilo.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa sasa wananchi kutoka wilaya hiyo waliokuwa wakifanya shughuli za kilimo katika taifa hilo la jirani na kuzuiwa kuingia kuvuna mashamba yao na viongozi wa Kenya hawatazuiliwa tena.

“Nimeongea na DC(Mkuu wa Wilaya) wa Kajihado kumueleza hizo kero mnazo kabiliana nazo na ameahidi kwamba ataenda kuzifanyia kazi mara moja, lakini pia nimeongea na mwenyekiti upande wa Kenya wa hiki kijiji ambacho mpo karibu nacho amenihakikishia usalama wenu” amesema Mwaisumbe.

Aidha Mwaisumbe amewataka wananchi wa Wilaya hiyo wanaoingia katika taifa hilo la jirani kufanya shughuli za kilimo na biashara kutii sheria na maelekezo yanayotolewa na viongozi wa Kenya ili kutokuwekewa vikwazo vya shughuli zao na kudumisha umoja na mshikamano ulioasisiwa na waasisi wa mataifa hayo mawali hayati Mwalimu Julius Nyerere na Jomo Kenyatta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live