Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC akabidhi fedha kutengeneza viti vipya 108 vya Sekondari Sinon

268474d455bbc394a9f7b6082e1b4260 DC akabidhi fedha kutengeneza viti vipya 108 vya Sekondari Sinon

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa wilaya ya Arusha ,Kenani Kihongosi amekabidhi Sh milioni 5.3 kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Sinon Jijini Arusha, Nteles Lorna kwa ajili ya kutengeneza viti vipya 108 vilivyouzwa kama chuma chakavu kwa wafanyabiashara

Akikabidhi fedha hizo jana ofisini kwake, Kihongosi aliwaonya wafanyabiashara wa vyuma chakavu kuacha tabia ya kununua vitu ambavyo ni mali ya serikali.

Alisema fedha hizo zimechangwa na wazazi, walezi wa watoto pamoja na wafanyabiashara wa vyuma chakavu na kuongeza kuwa serikali inatoa fedha nyingi kuhakikisha watoto wanapata elimu hivyo kitendo cha kuiba viti ni cha kusikitisha na ni uhujumu uchumi.

Aliwataka pia watendaji wa kata ,wajumbe wa serikali za mtaa na mwenyeviti wa mtaa kuhakikisha watoto wanaokuwa mitaani wanakwenda shule kwa sababu wazazi wanawatumia kwenda kuuza vyuma.

Chanzo: habarileo.co.tz