Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC aitaka TFS kuhakikisha miche 111,000 ya miti inapandwa

09cc76f584f88fbf25b4233cb6db32e5 DC aitaka TFS kuhakikisha miche 111,000 ya miti inapandwa

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Colors Misungwi amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Msongela Palela kushirikiana na madiwani na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha miche 111,000 inapandwa katika vijiji vyote vilivyopo wilayani humo.

Wilaya ya Kalambo ilianzishwa miaka nane iliyopita baada ya kumegwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na ina vijiji 111.

Aidha alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Daud Sichone na madiwani wote 31 waoneshe mfano kwa kupanda miti katika makazi yao.

“Wilaya yetu kila mwaka inakubwa na maafa yanayosababishwa na kuvuma kwa upepo mkali, watu wanakosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na upepo mkali kisa watu wanakata miti hovyo ... madiwani anzeni kupanda miti katika makazi yenu pia wahimizeni wananchi kila kaya ipande miti minne katika makazi yake miti miwili mbele na miwili mingine nyuma ya nyumba na waitunze,” alisisitiza.

Misungwi alitoa kauli hiyo wakati akitoa salamu na maelekezo ya serikali katika kikao maalumu na madiwani wateule 31 walikula kiapo mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Kalambo, Ramadhani Rugemalira.

Madiwani hao walimchagua Daud Sichone (CCM) kuwa Mwenyekiti wa Halmashuri hiyo na Legius Boimanda (CCM) katika kikao cha baraza maalumu la madiwani lililoketi jana katika mji mdogo wa Matai.

Chanzo: habarileo.co.tz