Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC ahimiza kuendelezwa kwa amani kufanikisha utalii

C5ed09d4c69d6e9f8c80b90de54a5701 DC ahimiza kuendelezwa kwa amani kufanikisha utalii

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATANZANIA wametakiwa kuendelea kuilinda na kudumisha amani iliyopo chini ili iwe sehemu ya kuwavutia wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani kutembelea vivutio vya utalii hususan Mlima Kilimanjaro.

Aidha watanzania wametakiwa kuzilinda rasilimali zilizopo nchini ili ziweze kudumu kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.

Mkuu wa wilaya ya Moshi, Alhaji Rajab Kundya alitoa rai hiyo wakati akipokea timu ya watu 39 waliopanda mlima Kilimanjaro kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 Uhuru.

Miongoni mwa waliopanda mlima huo mrefu kuliko yote Barani Afrika ni wanahabari, watumishi wa hifadhi ya mlima huo, Shirika la Hifadhi za Taifa na wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ).

Kundya alisema amani iliyopo nchini inachangia kuwavutia watalii na kutaka ilindwe huku akiitaka jamii kuwafichua wanaohujumu rasilimali na maeneo yaliyohifadhiwa.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Alan Kijazi, Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho alisema watahamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii.

Aidha Batiho alisema Tanapa itaendeleza utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo, kulinda na kudumisha miundombinu ya Hifadhi.

Kiongozi wa Msafara huo wa watu 38, Kanali Msumari alisema wataendelea kulinda rasilimali za nchi hii na kuwataka watanzania pia kuzilinda rasilimali hizo. Alitaka asasi nyingine kuunga mkono utalii ikiwemo kupanda Mlima Kilimanjaro.

Chanzo: habarileo.co.tz