Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC afuta vibali ukataji miti

Forest G4c7d3518a 1920 DC afuta vibali ukataji miti

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro, Dustan Kyobya amefuta vibali vyote vya kukata miti katika wilaya hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ofisi yake, Kyobya alisema kwa kuzingatia umuhimu wa mazingira watu wamekuwa wakikata miti ovyo hivyo ameamua kuchukua hatua.

Alisema kwa mujibu wa sheria hauruhusiwi kukata miti bila kibali cha mkuu wa wilaya hivyo baada ya kuwasili katika wilaya amesitisha utaratibu wote wa kukata miti hadi pale atakapojiridhisha.

Alieleza kuwa kwa sasa mwananchi yeyote anayetaka kukata mti hata kama amepanda mwenyewe atatakiwa kuandika barua kuanzia serikali za mitaa au kijiji na kuipeleka kwenye ofisi za Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ambao watamshauri mkuu wa wilaya.

“Nitajiridhisha mwenyewe pale ambapo tutaona ni lazima kweli kwa mti kukatwa ikiwa utakuwa unahatarisha maisha ya mtu au kuharibu nyumba ndipo tutatoa kibali cha kukata mti,” alisema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live