Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC acharuka viwanja vya ndege kugeuzwa barabara

Airports Nnnnnnnnnnnnnnnnnn Acheni kugeuza uwanja wa ndege kama barabara

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa mtaa wa Idundilanga Halmashauri ya mji wa Njombe wameitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusu kuanza ujenzi wa Uwanja wa ndege uliopo mjini humo ili kuwaepusha na kero inayowatesa muda wote ya kukabwa na vibaka 

Wakitoa kero zao katika mkutano ,wakazi  wamesema  wanapata shida kubwa kwasababu kukosekana kwa vituo vya basi katikati ya mji pamoja na kukamatwa na kulipishwa faini kwasababu ya kukatisha katika uwanja wa ndege uliyopo mjini Njombe ambao wanasema  hautumika ipasavyo na ndege hivyo wanaomba serikali ione namna ya kutatua adha hizo.

Akijibu kero hizo Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa amesema tayari serikali imekamilisha mchakato wa awali ujenzi wa  uwanja wa  ndege wa mkoa wa Njombe na kisha kutoa onyo kwa wanaotumia uwanja huo kinyume  na  taratibu kwasababu ni kosa kisheria .

Aidha mkuu wa wilaya ya Njombe ametoa onyo kwa watendaji wazembe wanaoshindwa kutekeleza maagizo ya serikali ,kwamba haitasita kuwapeleka pembezoni mwa miji na kuwaleta mijini wanaofanya kazi kwa bidii ili kujifunza kwao.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live