Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC aagiza TAKUKURU imchunguze Mkurugenzi

Mkuu Wa Wilaya Ya Geita, Colnery Magembe.jpeg DC aagiza TAKUKURU imchunguze Mkurugenzi

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Colnery Magembe ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita kuhakikisha inachunguza safari za Mkurugenzi wa Halmashauri Ya Mji Geita, Zahara Michuzi kama zina tija kwa Halmashauri na Serikali kiujumla.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kulalamikiwa kutoonekana kwenye vikao muhimu na badala yake kukaimisha Maofisa wanaoshindwa kutoa majibu sahihi katika vikao hivyo.

Magembe ametoa maagizo hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji Geita ambapo amehoji sababu za kutokuwepo Mkurugenzi wa Halmashari na kufahamishwa yupo nchini China.

“Nawashukuru Mwenyekiti na Madiwani kama mnaweza kumtuma Mkurugenzi kwenda China kujifunza kwa ajili ya kuja kufundisha lakini elimu atakayoipata ije ioneshe kweli, isiwe sasa kichaka eti kwasababu wewe ni Mkurugenzi unaweza ukaamua leo ukafanya safari ya kwenda tu, kwa matumizi ya kutumia hela ya Halmashauri.”

“Na hili ninaomba TAKUKURU mfuatilie hiyo safari kama ilikuwa ni kwa maslahi ya Halmashauri na kwamba kuna hela ilitumika kwa maslahi ya Halmashauri kama safari ile haikuwa kwa maslahi ya Halmashauri na zimetumika fedha za Halmashauri kwa maslahi ambayo siyo ya Halmashauri fedha zile zirudishwe zikafanye kazi nyingine.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live