Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Warioba aagiza watumishi wote kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura.

80440 Dcpic%255C

Thu, 17 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mkuu wa wilaya ya Moshi (DC) mkoani Kilimanjaro, Kippi Warioba ameiagiza halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha watumishi wote wa idara mbalimbali wanajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kuelekea  uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.

Warioba ametoa agizo hilo leo Jumatano Oktoba 16, 2019 wakati alipotembelea halmashauri hiyo.

"Pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha na nyie hakikisheni watumishi wote wanajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kwani zoezi hili ni muhimu kwa kila mmoja wetu," amesema Warioba wakati alipokuwa akizungumza na mawakala.

Aidha Warioba amekipongeza Chuo cha Ushirika Moshi kutokana na kasi kubwa ya uandikishaji wa wanafunzi katika daftari la mpiga kura.

"Nimeridhishwa na kasi yenu endeleeni kuhamasishana mpaka ikifika kesho muwe mmezidi idadi hii ya watu 600 ambayo mko nayo leo, "amesema Warioba

Naye Rais wa chuo hicho, Yesaya Melita amesema bado wanaendelea kuhamasisha wanafunzi kujitokeza kwa wingi na kwamba mpaka sasa wana idadi ya wanafunzi 600 ambao tayari wameshajiandikisha.

Pia Soma

Advertisement
NEC yabaini Watanzania wengi wamepoteza kitambulisho cha mpiga kura

Chanzo: mwananchi.co.tz