Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC: Wapokeeni watoto hata bila sare

3ab1e7d496b99c6c3586b6442b6896b1 DC: Wapokeeni watoto hata bila sare

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Said Mtanda, amewapa siku saba wanafunzi 1,641 wawe wamejiunga kidato cha kwanza kwenye shule walizopangiwa.

Aliagiza walimu wakuu wawapokee wanafunzi hao hata kama hawana sare za shule na wanatembea bila kuvaa viatu.

"Wabunge, madiwani, wataalamu, maofisa elimu kata, maofisa tarafa, watendaji wa vijiji na kata pia Ofisa Elimu Elimu ya Msingi Wilaya wahakikishe wazazi na walezi watoto wao wanaripoti shuleni kwa wakati vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao" alisema Mtanda.

Alitoa maelekezo hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari na wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza wilayani humo.

Alisema, wanafunzi ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza katika shule walizopangiwa wilayani humo tangu zifunguliwe Januari 11 mwaka huu ni sawa na asilimia 40 ya wanafunzi 4,301 waliochaguliwa.

Kuhusu miundombinu ya vyumba vya madarasa alisema, wilaya hiyo haina changamoto ya upungufu kwa kuwa mwaka uliopita ujenzi wa majengo 560 ya shule za msingi na sekondari ulikamilika.

Chanzo: habarileo.co.tz