Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Victoria awapa tahadhari wanufaika fidia mradi wa Mchuchuma

DC Victoria Awapa Tahadhari Wanufaika Fidia Mradi Wa Mchuchuma DC Victoria awapa tahadhari wanufaika fidia mradi wa Mchuchuma

Thu, 18 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amewataka wakazi wa kata ya Nkomang’ombe wilayani humo ambao wanaenda kunufaika na fidia ya malipo ya kupisha mradi wa Mchuchuma kufanya matumizi yenye tija ili waweze kujipatia maendeleo pasipo majuto yoyote.

Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata hiyo uliohusisha viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya Mkoa, wilaya sambamba na viongozi wa chama wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka.

Mwanziva amesema wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Sh. Bl. 5.2 za kuwalipa wananchi hao Nkomang’ombe hivyo wananchi wanapaswa kuzitumia vyema katika kukuza uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.

“Mama Samia amefanya mambo mengi sana hapa Ludewa, wananchi mlikuwa na manung’uniko juu ya fidia zenu hivyo kwa kutambua uhitaji na umuhimu wenu mama sasa kawaletea hayo mabilioni ya fidia mliyokuwa mkiyaota usiku na mchana hivyo tunapaswa kumshukuru haswa! Rais wetu”.

Aidha, kwa upande wa wanachi hao ambao wameonekana kujawa na furaha kwa kufikia hatua hiyo kwani kilio hicho kilikuwa ni kilio cha miaka mingi na walikuwa wakiona kuwa ni ndoto huku wakihoji juu ya upataji huduma katika maeneo wanayoenda kupelekwa kwakuwa kuna baadhi ya maeneo hayo wamepelekwa watu wachache na wengine wakihoji juu ya hatma ya mazao yao waliyolima.

Stephano Mhagama ni miongoni mwa wananchi hao amesema katika maeneo mengine wamepelekwa wananchi wengi zaidi na mengine wachache hivyo wanahofia huko walikopelekwa wachache endapo wataletewa huduma stahiki kama Afya, maji.

“Kuna wenzetu wa kijiji cha Idusi ambao wako wengi wote kwa pamoja wanahamishia eneo moja ambalo wanaenda kuanzisha maisha huku sisis wengine wa kijii cha Nkomang’ombe tuko wachache tuu tunaopisha mradi huu nasi tumepelekwa huko kwa makazi mapya sasa hofu yangu huko tunakoenda serikali itatulete huduma muhimu ilihali tuko wachache?,” amesema Mhagama.

Hata hivyo, swali hilo linajibiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ambaye hapo awali alikuwa afisa ardhi wilayani humo kwa kusema kwamba kila mwananchi ana hakibya kuishi mahala popote hivyo endapo mwananchi hatoridhia kwenda eneo analopelekwa anaweza tunza eneo hilo na kutafuta eneo jingine litakalo mfaa kuweka makazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live