Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Ubungo ampongeza Rais Samia kuidhinisha Bil. 65 za maji

Thumb 1214 800x420 0 0 Auto DC Ubungo ampongeza Rais Samia kuidhinisha Bil. 65 za maji

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Taifa linaadhimisha miaka 61 ya Uhuru, Mkuu wa Wilaya Ubungo Mhe. Kheri James amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuidhinisha zaidi ya bilioni 65 kuboresha huduma ya maji katika wilaya ya Ubungo.

Ameyasema hayo wakati akitoa mada kwenye mdahalo wa miaka 61 ya Uhuru wa nchi ulioandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika miaka hii 61, katika Wilaya ya Ubungo Serikali imewezesha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ikiwemo huduma ya maji, elimu na afya pia alichukua nafasi hiyo kuwapongeza DAWASA kwa kuhakikisha wilaya ya Ubungo inapata huduma ya majisafi na kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati kwa maeneo ambayo hayajapata huduma.

Mhe. James amesema kuwa Serikali imefanikiwa kutatua changamoto ya huduma ya majisafi katika Wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza mradi wa Shilingi bilioni 65.4 pamoja na mradi wa Mshikamano ambayo yote inakamilika mwezi huu wa Disemba na kutoa huduma kwa wananchi wote wa Ubungo, Goba ,Kibamba, Saranga na Mbezi.

"Nipende kumshukuru sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za miradi ya maji ambayo ikienda kukamilika itagusa maeneo mengi katika wilaya ya Ubungo yenye changamoto ya maji pamoja na miradi ya Elimu na afya ambazo ni huduma muhimu kwa jamii," ameeleza Mhe Mkuu wa Wilaya.

Akitoa salamu kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja, Meneja wa DAWASA Kibamba Ndugu Elizabeth Sankere ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusimamia kikamilifu huduma ya maji kwa wananchi wote kupitia DAWASA ambapo mpaka sasa huduma ya maji inapatikana kwa zaidi ya asilimia 90 kulinganisha na hali ilivyokuwa awali.

Ameeleza kuwa huduma ya maji kwa Wilaya ya Ubungo kwa sasa imeimarika na kazi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji inaendelea ili kila mkazi wa Ubungo apate huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live