Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC: Toeni taarifa fedha ujenzi wa madarasa

C6d20eda5c51c5ee180e6aff0a0c0505 DC: Toeni taarifa fedha ujenzi wa madarasa

Sun, 21 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Ilemela, Dk Mathias Lalika ametaka wananchi wapewe taarifa za matumizi ya fedha wa ujenzi wa madarasa kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Alitoa rai hiyo wakati akikagua ujenzi wa madarasa, vyoo, ofisi za walimu, viti na meza akiwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.

Aliwaagiza walimu wakuu na kamati za ujenzi, kutumia vizuri fedha zilizotolewa na Serikali na michango ya wananchi kukamilisha miundombinu hiyo ya madarasa.

Alitaka kuwepo kwa ushirikishwaji na uwazi ili kuondoa taharuki mbalimbali kwa wananchi.

Kaimu Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ilemela, Alex Mkusa alisisitiza kamati za ujenzi za shule kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati kwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imeshatenga fedha zote kwa shughuli zinazoendelea.

Alisema awamu ya kwanza ya fedha hizo, imeshawekwa kwenye akaunti za shule zote zenye miradi ya ujenzi wa madarasa.

“Ujenzi huu ni budi ukamilike kwa wakati kwani hatuna kizuizi, mahitaji yote yapo na pesa ipo, hivyo kila shule mfanye juhudi kukamilisha ujenzi wa madarasa haya kwa wakati kwani shule zetu zote zimepangiwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na shule zimeshafunguliwa.Tukamilishe mradi huu kwa wakati na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,”alisema Mkusa.

Manispaa Ilemela kupitia mapato yake ya ndani, imetoa Sh milioni 252 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 60 kwa shule 16 za sekondari kwa awamu ya kwanza.

Chanzo: habarileo.co.tz