Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Temeke atoa somo kwa wenye watoto viziwiwasioona

73216 Sensapic

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke (DC), Dar es Salaam nchini Tanzania, Felix Lyaniva amewataka wazazi na walezi wilayani humo kutowaficha watoto wenye ulemavu wa kusikiakutoona bali wajitokeze kuwapeleka katika vituo vya afya ili waweze kupewa huduma.

Lyaniva alisema hayo jana Jumanne Agosti 27, 2019 wakati akizindua kituo cha kutoa afua za mapema kilichojengwa na Shirika la Sense International Tanzania katika Kituo cha Afya Yombo Vituka.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwa mara ya kwanza alipoelezwa kuhusu visiwiwasioona hakuelewa hadi alipoeleweshwa.

“Kwangu ilikuwa kitu kigeni kabisa, mimi najua kuna kiziwi lakini kiziwiasiyeona nilikuwa sijui, nilishtuka na nashukuru sana sasa nafahamu,” alisema

Alilipongeza shirika hilo kwa kujenga vituo vinne katika wilaya yake na kuwaomba kama inawezekana vijengwe katika vituo na zahanati zote za wilaya hiyo.

Alisema Kituo cha Yombo Vituka wanakusudia kukipandisha hadhi na kuwa Hospitali ya Wilaya baada ya ile ya wilaya kupandishwa hadi kuwa Hospitali ya Rufaa.

Pia Soma

Alisema wale wazazi wote ndani ya wilaya ya Temeke wenye watoto viziwikutoona wajitokeze na kuwapeleka katika vituo hivyo vya Yombo Vituka, Mbande, Hospitali ya Rufaa Temeke pamoja na Mbagala- Round Table.

“Wale wote ambao wamejaaliwa kuwa na watoto viziwiwasioona wawapeleka katika vituo hivi ili wapatiwe huduma, ikibainika kuna mzazi kamficha mtoto tutamchukulia hatua,” alisema

“Watendaji wa ngazi zote katika wilaya yangu, hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa shirika hili ili kuwaleta na kupimwa watoto wote ili waelekezwe jinsi ya kuwahudumia kwani kuwa kiziwiusioona sio mwisho wa maisha.”

Mkuu huyo wa wilaya  alitoa agizo kuwa vikao vinavyofanyika vya kiutendaji kwenye  wilaya yake kuhakikisha wanajadili suala la viziwiwasioona na iwapo ikitokea akafuatilia na kubaini hawafanyi atawachukulia hatua.

“Mimi hili la viziwiwasioona nimelichukua, nitakuwa balozi mzuri kila nitakapokwenda na katika mikutano yangu ya hadhara nitalizungumza ili wananchi waweze kulielewa,” alisema Lyaniva

Awali, Mkurugenzi Mkazi wa Sense International, Naomi Lugoe alisema vituo hivyo vinne katika wilaya hiyo ni vya mfano na vina lenga kuwafikia watoto 72,000.

Alisema kila kitu0 kimejengwa kwa Sh60 milioni sawa na Sh240 milioni kwa vyote viwili huku gharama za vifaa  kwa kila kituo kimoja kikiwa ni Sh37.5 mlioni.

Lugoe alisema walemavu wa visiwikutoona, “wanapata shida sana kuishi katika mazingira yetu hivyo kuwafanya kuishi maisha magumu. Hawajui ni mchana wala usiku na hata kuwahudumia imekuwa changamoto.”

“Kutokana na hilo, Sense International ndipo linapoingia na kuanza kuwasaidia kuanzia wadogo na vituo hivi vitawezesha kuwapima watoto kuanzia mwaka sifuri hadi miaka sita na watakaobainika tutaanza kuwahudumia mapema,” alisema mkurugenzi huyo

Alisema mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Uingereza linaloitwa Jersey Oversea Aid (JOA) ambapo mafunzo yalitolewa kwa watu wanaotoa huduma kwenye vituo hivyo pamoja.

Naye Mwakilishi wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, John Makange alisema wizara inatambua mchango unaotolewa na Sense International kwani kwa vituo hivyo, “itafungua fursa kwa watoto wengi kupata huduma ambayo bila hivyo wangefichwa na wazazi au walezi bila kupata msaada.”

Makange ambaye pia ni Mratibu wa Huduma Mtengamano na Tiba Shufaa wa wizara hiyo alisema wizara iko tayari kutoa ushauri na miongozo ili kuhakikisha malengo  yaliyokusudiwa yanafikiwa.

“Tunawaomba wazazi na walezi kuwaleta watoto kutambulika ikiwa watagundulika wana tatizo la kusikiakuona ili waweze kupata huduma hii mapema,” alisema

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Sense International, Rutachwamagyo Kaganzi alisema kuna ulemavu tofauti tofauti, “lakini kundi la visiwikutoona wana hitaji msaada zaidi.”

“Mtu anahitaji milango mitano ya kupashana habari, wao wana milango mitatu tu hivyo wanahitaji sana msaada wa kusaidiwa,” aliongeza

 

 

 

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz