Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva ameomba tamasha la utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest) kufanyika kwa siku moja zaidi.
Lyaniva ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 28, 2019 alipokuwa akizungumza katika kilele cha tamasha hilo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Amesema maonyesho hayo yakiendelea hadi kesho yatawapa fursa walio kazini kuhudhuria na kupata bidhaa.
“Mgeni rasmi tunaomba tamasha lisogezwe hadi kesho watu wengi wapate fursa ya kujionea vizuri tulivyonavyo,”
“Maonyesho haya tumejifunza mengi, tamasha limefana, Dar es Salaam ilikuwa shwari wageni wameishi kwa amani. Nimeona watu wamebadilishana mawasiliano ikiwa ni kibiashara ni sawa hata kama uchumba. Mtanzania mzuri ruksa kuoa na kuolewa hayo ndiyo mahusiano mema, ” amesema Lyaniva.