Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Tanga: Msiwafunge watoto hirizi, wapelekeni hospitali

Hirizi Watoto Watoto (600 X 360) Msiwafunge watoto hirizi, wapelekeni hospitali

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: Habarileo

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amewataka Wazazi kuwapeleka Hospitali Watoto wanaozaliwa wakiwa na changamoto kama vile kuwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi badala ya kuishia kuwafunga hirizi na kubaki nao nyumbani.

"Kuna wakati unaona Mtoto kazaliwa akiwa na changamoto tamaduni zetu baadhi yao unakuta Mtoto badala ya kupelekwa Hospitali amekimbizwa kufungwa mahirizi miguuni na shingo tuondokane na hizo dhana badala yake tuwapeleke Watoto Hospitali ili wapatiwe matibabu”

Mgandilwa amesema hayo Tanga kwenye maadhimisho ya siku ya Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Kiwilaya, ambapo kitaifa yafanyika kesho October 25,2022.

Chanzo: Habarileo