Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patrick Sawala amewa hamasisha wananchi wilayani humo kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa corona ili kujihakikishia usalama zaidi wa afya zao.
Awali wilaya hiyo imejiwekea mikakati ya uchanjaji ambapo kwenye kila mikusanyiko ya watu huduma hiyo hutolewa.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mesema kuwa mpaka sasa hakuna mgojwa wa corona katika wilaya hiyo.
“Sisi sio kisiwa kwa thutadhibiti wageni hapa lakini tuendelee kuchukua tahadhari na kusikiliza maelekezo ya Wizara ya Afya nendeni mkachanje msiache. Kuchanja ni muhimu sana kwa afya zetu na familia zetu”
“Tunapohamasisha mkachanje sio kwa faida yetu hapana na kwako pia kuna wakati hii chanjo hautaipata na kibaya zaidi ni kwamba ugojwa huu unanatunyemelea hasa sisi ambao umri umeenda. Nendeni mkachanje ili kujiweka katika usalama zaidi” alisema Sawala