Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Tabora aingilia kati mgogoro wa ardhi shule ya Milambo na wananchi

DC Tabora Aingilia Kati Mgogoro Wa Ardhi Shule Ya Milambo Na Wananchi.jpeg DC Tabora aingilia kati mgogoro wa ardhi shule ya Milambo na wananchi

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya Tabora Deusdedith Katwale ameunda tume kuchunguza mgogoro uliopo baina ya Shule ya Sekondari Milambo na wananchi wanaozunguka shule hiyo kufuatia mgogoro wa ardhi uliopo baina yao.

Tume hiyo itakayofanya kazi kwa siku saba itaongozwa na kamishina wa ardhi na wajumbe kutoka ofisi ya DSO, Takukuru, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa.

Katwale ametoa maagizo hayo baada ya kufika katika eneo hilo na kuzungumza na wananchi,ambapo alipokea taarifa ya nyumba zaidi ya 30 zinazodaiwa kujengwa ndani ya eneo la shule..

DC Katwale amewataka wananchi wa maeneo hayo kuendelea na shughuli zao wakati tume ikiendelea kuchunguza jambo hilo na kusema maamuzi yatakayofanyika yatazingatia haki kwa pande zote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live