Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Simanjiro awataka wazazi, walezi kupeleka vyakula shuleni

90943 Pic+simanjiro DC Simanjiro awataka wazazi, walezi kupeleka vyakula shuleni

Mon, 6 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Wakati shule zimefunguliwa sehemu mbalimbali nchini Tanzania leo Jumatatu Januari 6, 2020 wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, wametakiwa kuhakikisha wanapeleka vyakula pindi watakapowafikisha watoto wao shuleni.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro (DC) mkoani Arusha, Zephania Chaula ametoa agizo hilo leo Januari wakati akizungumzia suala zima la upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wa shule zilizopo katika wilaya hiyo.

Chaula amesema kutokana na jiografia ya umbali mrefu katika ya shule na makazi, inawabidi wanafunzi wapatiwe chakula pindi wakiwa shuleni, kuliko kwenda kula na kurudi shule.

Amesema kutokana na umbali huo, ameshaagaza wazazi na walezi kuchangia chakula ili watoto wao waweze kula shuleni na kuongeza kiwango cha taaluma shuleni.

"Walimu hawapaswi kushika fedha au kuwa kwenye kamati za fedha za chakula, kuna mwongozo wa serikali unatamka hilo, ila wazazi na walezi pekee ndiyo wenye kutakiwa kusimamia," amesema Chaula.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi amesema wanafunzi 4,496 wameandikishwa kuanza darasa la kwanza.

Myenzi amesema shughuli ya uandikishaji inafanyika kwa muda wa miezi mitatu hivyo uandikishaji unaendelea kwenye shule mbalimbali.

Amesema hawana tatizo la upungufu wa madarasa ya watoto kusoma hivyo wanaendelea kukagua utaratibu wa uandikishaji wanafunzi ili waweze kusoma kwa ufanisi.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mirerani, Tenisia Elias akizungumza na wazazi na walezi waliowapeleka watoto wao shule amesema wanapaswa kuandikisha kwa mtendaji wa kitongoji.

Mwalimu Elias amesema wazazi na walezi wanapaswa kuandikisha majina ya wanafunzi kwa watendaji ambao nao wanafikisha majina yao kwenye shule hiyo.

"Pamoja na hayo wazazi na walezi huwa mnafika kwenye mikutano ya vitongoji mnatangaziwa kuja na vyakula ili watoto wale shuleni lakini sioni mmebeba vyakula," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz