Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Sengerema atoa saa 24 walijenga mabondeni kuondoka

85624 Pic+dc DC Sengerema atoa saa 24 walijenga mabondeni kuondoka

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sengerema. Mkuu wa Wilaya ya Sengerema (DC) jijini Mwanza, Emmanuel Kipole ametoa saa 24 kwa wakazi wote wilayani huyo waliojenga kwenye mabonde pamoja na mito kuondoka ndani ya muda huo na atakaye kaidi atachukuliwa hatua za kisheria.

DC Kipole ametoa agizo hilo jana usiku Jumamosi Novemba 23, 2019 alipofanya doria akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya baada ya kutokea vifo vya watu kumi vilivyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Alisema watangulizi wake walikuwa wamekwisha toa tamko la watu hao waliojenga bondeni kuondoka lakini walikaidi.

"Sitavumilia hali hii, sina mzaha na hili lazima waondoke wakatafute viwanja maeneo mengine ambayo siyo hatarishi," alisema Kipole.

Mmoja wakazi wilayani huyo, Musa Mtu alisema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inatakiwa kuchukua uamuzi ya haraka kuvunja nyumba zote zilizojengwa kando ya mto huo kwa kuwa zinasababisha sehemu kubwa maji kutokupita kwenye mto huo.

Matukio ya watu kusombwa na maji na wengine kufariki dunia kwa kuangukiwa na nyumba yamekuwa yakitokea mara kwa mara wilayani humo hasa kipindi cha mvua.

Chanzo: mwananchi.co.tz