Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Same ataka vijana waliofaulu mgambo kupewa kipaumbele

DC Same Ataka Vijana Waliofaulu Mgambo Kupewa Kipaumbele DC Same ataka vijana waliofaulu mgambo kupewa kipaumbele

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameutaka uongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na viongozi wengine wa taasisi za Umma na binafsi kutoa kipaumbele kwa vijana waliofudhu mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) kuimarisha ulinzi na shughuli nyingine za ujenzi wa Taifa.

Ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo kwa askari 106 wilayani humo akiwataka askari hao kuzingatia kiapo na kuwa mstari wa mbele kupambana na maovu.

“Niwahakikishie vijana wetu serikali itaweka kipaumbele kuhakikisha inapotokea fursa yoyote mnapewa kipaumbele iwe shughuli zilizo Chini ya Halmashauri ikiwemo Ulizi, kusimamia makusanyo ya mapato, kukimbiza mwenge na nafasi za JKT mnachopaswa kuzingatia ni uadilifu na kuviishi viapo mlivyo apa baada ya kuhitimu mafunzo,” alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Amewataka pia wahitimu hao kuangalia uwezekano wa kuniendeleza kielimu kwa kusoma kozi mbalimbali ikiwemo Udereva, ufundi Umeme na Uwashi kujijengezea ujuzi na sifa za kuwa na vyeti ambavyo vitawasaidia kipindi zitakapo tokea nafasi za ajira serikini kupewa kipumbele kwa kuwa na sifa za ziada.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live