Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Sabaya afikishwa kwa RC Mghwira

37362 Pic+sabaya DC Sabaya afikishwa kwa RC Mghwira

Sun, 20 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Sakata la Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Yohana Sintoo na Mwenyekiti wa Halmashauri, Helga Mchomvu kufukuzwa na mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya kwenye ukumbi wa halmashauri, limefikishwa kwa mkuu wa mkoa huo, Anna Mghwira.

Sabaya aliwatimua ukumbini mkurugenzi na mwenyekiti hivi karibuni wakati viongozi hao wakiongoza kikao cha kamati ya fedha ya wilaya hiyo.

Akizungumzia hatua waliyochukua leo Ijumaa Januari 18, 2019, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Helga Mchomvu amesema moja ya ajenda zilizokua zikijadiliwa katika kikao kile ni hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambazo zilitakiwa kujibiwa katika kikao kile licha ya mkuu wa wilaya kukivuruga na kuwasababishia hasara na gharama kubwa za kukirudia kikao hicho.

Mchomvu amesema suala hilo wameshalipeleka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mghwira na endapo halitapatiwa ufumbuzi watalifikisha kwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo.

"Bado tunausubiri mrejesho kutoka kwa mkuu wa mkoa na kama tusipopata majibu tutaenda mbele kumuona waziri husika," amesema Mchomvu.

"Tunataka tupate sababu za msingi ni kwa nini DC Sabaya alivuruga kikao kile na kuingia kwenye kikao cha kamati ya fedha ambacho kilikua ni siri na kuingiza wananchi tofauti na utaratibu," amesema Mchomvu.



Chanzo: mwananchi.co.tz