Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amemaliza mgogoro wa upotevu wa fedha kiasi cha Sh76.9 milioni za wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Moshi uliodumu zaidi ya mwaka mmoja.
Akizungumza leo Jumatano Oktoba 2,2019 Sabaya amesema tayari Sh56 milioni zimeshatolewa na wahusika na kwamba, wanafunzi wataendelea na masomo bila kikwazo.
Amesema wahusika waliokuwa wanadaiwa fedha hizo ni aliyekuwa mweka hazina wa chuo hicho Sarafina Mbwambo ambaye amelipa Sh10 milioni kati ya Sh20 milioni anazotakiwa kuzilipa.
Wengine waliorejesha ni wakala wa benki ya CRDB kupitia Saccos ELCT, Melkizedeck Mchau ambaye amelipa Sh20milioni kiasi chote ambacho alitakiwa kulipa.
Pia, chuo hicho kimelipa Sh12.3 milioni na benki ya CRDB imeahidi kulipa deni wanalotakiwa kulipa ndani ya wiki mbili kuanzia leo a ni Sh12.3milioni.
Naye Mkurugenzi wa chuo hicho, Joseph Mong'are alimshukuru Rais John Magufuli kwa jitihada za kuhakikisha fedha za wazazi wanyonge zinarudishwa kwa kuzingatia haki na usawa.
Pia Soma
- Waziri mkuu asema hospitali ya kanda itarahisisha huduma
- Mjasiriamali wa Arusha ashinda tuzo ya Citi Bank
- Naibu waziri Kandege atoa mwanga watumiaji mabasi yaendayo haraka Dar