Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Odunga akata rufaa, apinga kutoa Sh7 milioni za matunzo ya mwanaye

83146 Pic+odunga DC Odunga akata rufaa, apinga kutoa Sh7 milioni za matunzo ya mwanaye

Fri, 8 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amekata rufaa Mahakama ya Wilaya Ilala akipinga hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga.

Katika hukumu hiyo, Odunga alitakiwa kutoa Sh7 milioni kama nusu ya gharama za matunzo aliyotumia mkewe, Medilina Mbuwuli kumsomesha mtoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

Odunga alifungua kesi kumtaliki mkewe lakini mahakama ililikataa ombi hilo, badala yake ikamtaka alipe kiasi hicho cha fedha.

Jana, Medelina alikwenda Mahakama ya Ukonga kujua utekelezaji wa hukumu hiyo na kukumbana na rufaa ya Odunga.

Katika hukumu ya Ukonga, Odunga pia alitakiwa kutoa Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mwanaye.

Kwa mujibu wa rufaa hiyo ambayo nakala yake ilipokelewa na Mbuwuli Novemba 5, itatajwa mahakamani hapo Novemba 19. Katika maelezo ya kukata rufaa, Odunga alidai kuwa hakimu aliyesikiliza kesi yake dhidi ya Medilina alifanya kosa kutamka amlipe Sh7 milioni.

Alisema hakimu huyo alifanya kosa kwa kutokutoa talaka na kubainisha kuwa ana imani ndoa yake haipo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 18 na Hakimu Christina Luguru baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili alisema mdaiwa aliiomba mahakama kuwa Odunga atoe nusu ya Sh13 milioni ambazo alitumia kumhudumia mtoto wao na aendelee kuwatunza yeye na mwanaye kwa kuwa bado ni mkewe.

Hakimu Luguru alisema sheria ya ndoa kifungu cha 63 inaeleza pamoja na kifungu cha 129 ni jukumu la baba kutunza mke na mtoto. Alisema kwa ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo, umeonyesha mtoto wao bado anasoma na mdai hakuwa akitoa matunzo hadi kupelekwa polisi.

Odunga hakuwa na ushahidi wowote kuonyesha alikuwa akilipa ada ila mdaiwa alipeleka risiti za ada mahakamani zikionyesha alilipa Sh14 milioni.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo alikuwa anadai kuwa mumewe hajawahi kutoa matunzo ya mtoto wao wa kike mwenye miaka 18 tangu akiwa chekechea hadi sasa yupo kidato cha sita.

SOMA ZAIDI Alisema licha ya mumewe kutotoa matunzo hayo, hayupo tayari kupewa talaka kwa sababu ndoa yao ni takatifu ya kanisani na bado anampenda mume wake na kwamba anajua hizo ni changamoto tu zimempitia.

Chanzo: mwananchi.co.tz