Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Nachingwea sasa aibeba ‘Furaha Yangu’

14594 Dc+pic TanzaniaWeb

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wilaya ya Nachingwea imepanga kuzindua kampeni ya upimaji wa hiari virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine mwanzoni mwa mwezi ujao, huku wanaume wakiwa walengwa wakuu.

Hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya kitaifa iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Majaliwa alisisitiza kuwa Serikali imeanzisha mkakati wa kutambua kiwango cha maambukizi kitaifa na hatimaye kuanza kutoa dawa za kufubaza makali ya Ukimwi kwa watakaobainika kuambukizwa.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango alisema alipotembelea ofisi za Mwananchi zilizopo Tabata relini jijini Dar es Salaam jana, kuwa kampeni hiyo itakayodumu kwa siku nane kuanzia Agosti Mosi, itahusisha upimaji wa maradhi mengine ikiwamo macho na saratani ya shingo ya kizazi.

“Kampeni hii ya Furaha Yangu itakuwa na siku ya uzinduzi na kilele. Pia, itafanyika bure tunaomba wananchi watumie fursa hii kupata elimu na kuhamasika kujua hali ya afya zao,” alisema Muwango.

Alisema kwa vile wanaume wamekuwa na tabia ya kuwategea wenza wao kujua afya zao, kampeni hiyo imelenga kuwahamasisha zaidi ili wajitokeze na kutambua afya zao.

Kuhusu kampeni iliyofanyika hivi karibuni wilayani humo ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, Muwango alisema imesaidia kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.

Alisema kabla ya hatua hiyo watoto wengi walikuwa wakipata shida na baadhi kuishia kwa waganga wa jadi, lakini sasa wameelimishwa kuhusu tatizo hilo na kufahamishwa kuhusu matibabu ya bure yanayotolewa katika Taasisi ya Mifupa ya Moi.

Chanzo: mwananchi.co.tz