Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kulipa kipaumbele swala la lishe katika jamii.
DC Mwenda ameyasema hayo, katika viwanja vya halmashauri wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe.
DC Mwenda amesisitiza umuhimu wa kuwa na bustani ya mbogamboga katika shule zote za msingi na sekondari zilizopo wilayani Iramba, ili kuwajengea wanafunzi utamaduni wa lishe bora kwa vitendo.
Aliongeza kuwa shughuli hizi zinapaswa kuanzia uzalishaji, uandaaji, na matumizi ya mboga mboga kwa wingi, hivyo kuitengeneza jamii inayojali afya bora kupitia lishe bora.