Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Musoma kufunga shule kwa kukithiri vitendo vya kishirikina

Mganga 1?fit=640%2C326 DC Musoma kufunga shule kwa kukithiri vitendo vya kishirikina

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: dar24.com

Mkuu wa wilaya ya Musoma, Vicent Naano ametoa wiki moja kwa Wananchi wa Kijiji cha Kakisheri wanaojihusisha na matukio ya kishirikina kuacha vitendo hivyo haraka na endapo vitandelea basi atafunga shule ya msingi Kambarage na kuwahamisha Walimu.

DC huyo ametoa agizo lenye onyo kwakuwa Shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na matukio yasiyo ya kawaida ikiwemo Walimu kuingiliwa kimwili nyakati za usiku, kulazwa nje na wanafunzi kudondoka hovyo na kupiga kelele.

Imeelezwa kuwa matukio ya wanafunzi wa darasa la 7 kuanguka  na kupiga kelele, kukuta chakula aina ya makande kikiwa kimewekwa chooni yaliwalazimu walimu, wazazi na wanafunzi kupiga kura ili kubaini anayefanya matukio hayo kwa imani ya kishirikina.

Rwanda yawanasa magaidi 57, wasombwa kutoka msituni

Chanzo: dar24.com