Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Muro ampongeza Magufuli

29826 MURO+PIC TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arumeru. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amemshukuru Rais John Magufuli  kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya maji, afya na elimu katika wilaya hiyo.

Akizungumza leo Jumapili Desemba 2, 2018 wakati akitoa salamu za wilaya hiyo mbele ya Rais Magufuli, Muro amesema Wilaya ya Arumeru imepata Sh3 bilioni katika mpango wa elimu bure na hivyo kuchangia kuongeza wanafunzi katika shule za msingi na sekondari.

Muro amesema wilaya  hiyo imepokea Sh500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya eneo la Nduruma, Sh104milioni ujenzi wa kituo cha afya Usa River na Sh400 milioni za mradi Mbuyuni.

Amedai kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Rais Magufuli akifika Arumeru atapunga mkono tu, bila kuzungumza kwani kazi zake zimeonekana.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz