Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Muro Anasa Mtandao wa Wizi wa Mifugo

Muro?fit=640%2C411&ssl=1 DC Muro Anasa Mtandao wa Wizi wa Mifugo

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MTANDAO wa wizi wa mifugo umenaswa wilayani Arumeru baada ya vijana wawili ambao wanatajwa kuongoza mtandao huo kutiwa mbaroni.

Vijana hao wanadaiwa kuongoza uvunjaji wa mabanda na mazizi ya wananchi na kisha kuiba ng’ombe na mbuzi na kuchinja usiku ambapo alfajiri hupeleka nyama mabuchani.

Mtandao huo umenaswa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kufanikiwa kuwadaka vijana hao wakiwa na pikipiki mbili wakitupa ngozi pamoja na kitoto kichanga cha ng’ombe kilichofia tumboni baada ya kuchuna ngozi.

Alisema ameamua kuendesha msako huo baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa wafugaji waliodai mifugo yao kuvamiwa nyakati za usiku na kwenda kusikojulikana.

Chanzo: globalpublishers.co.tz