Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Mtatiro ataka polisi kutokimbizana na bodaboda kuepusha ajali

74749 Boda+pic

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amepiga marufuku tabia ya polisi kukimbizana na bodaboda na badala yake amewataka wachukue namba za vyombo hivyo na kuwaita vituoni dereva au mmiliki.

Amesema njia hiyo itawezesha madereva wanaokiuka sheria kuchukuliwa hatua bila polisi kuwakimbiza jambo ambalo linaweza kusababisha ajali.

Mtatiro ametoa uamuzi huo jana Jumamosi Septemba 7, 2019  katika kikao cha kuweka sawa mvutano kati ya polisi na bobaboda unaofukuta wilayani humo.

Mgogoro huo uliibuka Septemba 6, 2019 na kusababisha polisi wakabiliane na vijana wa bodaboda na kuwapiga mabomu ya machozi huku baadhi wakikamatwa.

Kufuatia mgogoro huo Mtatiro aliyekuwa ziarani wilayani Songea alilazimika kukatisha ziara hiyo na kuitisha kikao cha dharura katika kituo cha polisi na viongozi wa bodaboda.

Mtatiro ametumia fursa hiyo kuwaonya vijana wa bodaboda na kuwataka wafuate sheria, wakisimamishwa na polisi wasimame na kutoa ushirikiano.

Pia Soma

Advertisement

Pia amewataka polisi wasitumie nguvu bila sababu wakati wa kukabiliana na wananchi akitolea mfano  wa mabomu kutumika kuwasambaratisha bodaboda hao.

“Rais Magufuli (John) hataki kuona vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa wananyanyaswa na kupigwa maana ni vijana hao ndiyo watakaoipigia kura CCM na kuirejesha madarakani na kwamba kuwanyanyasa kunaenda kinyume na malengo ya CCM ya kuwalinda vijana,” amesema Mtatiro katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika mkutano huo, Mtatiro alifanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kumuomba ufafanuzi juu ya maelekezo yake ya makosa ambayo polisi hawapaswi kuyatumia kuwakamata madereva wa bodaboda na bodaboda zao.

Kikao hicho kilimaliza mvutano huku polisi na madereva bodaboda wakikubaliana kuwa bega kwa bega.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz