Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amerejesha shilingi milioni 85.4 (85,463,848) ambazo Wananchi waliporwa na Watu au Taasisi mbalimbali kinyume cha Sheria na kisha Ofisi ya DC Mtatiro ikafanya oparesheni za kuokoa fedha hizo.
Shilingi 44,272,196 kati ya tzs 55,535,497.69 zimerejeshwa kwa Wakulima waliokuwa wameporwa na Vyama vya msingi baada ya Wakulima kuuza mazao kwa mfumo wa stakabadhi za ghala kisha Watumishi wasio waaminifu wa baadhi ya Vyama vya msingi kuwadhulumu Fedha hizo.
Shilingi 12,000,000 kati ya 96,000,000 alizodhulumiwa Mwalimu Mstaafu Yusuph Bakari Yusuph baada ya kuwa amekopa 3,300,000 kwa Watu wawili binafsi na Taasisi moja ya ukopeshaji fedha ambapo pensheni yake ya Milioni 96 ilipoingia kwenye akaunti yake Watu hao wawili na Taasisi hiyo wanadaiwa kumteka na kumpeleka mjini kwa mujibu wa DC.
“Baadae walifanya connection Benki na kumpora Tsh. 63 Milioni huku kampuni ya ukopeshaji ikachukua milioni 33 kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 14 – 18 Feb 2019′-DC Mtatiro
Mzee aliripoti polisi lakini hakusaidiwa, miaka miwili baadaye mwezi Julai 2021 Mstaafu huyo alimfikishia suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru baada ya kukwama kwenye njia nyingine na ndipo nikachukua hatua na fedha zake zimeanza kurejeshwa baada ya hao waliomuibia kukiri kuwa walimdhulumu” —asema DC Mtatiro.
“DC Tunduru pia amerejesha Shs 18,381,456 kwa Wanachama wa TUNDURU TEACHERS SACCOS baada ya kutapeliwa na Vipngozi wao, pesa hizi ni 15% tu ya pesa zote wanazopaswa kulipwa, tunaendelea na kazi ya kusimamia hadi wote walipwe fedha zote”
Shilingi Mil 10,810,186 zimerejeshwa pia kwa Wananchi wengine mbalimbali na taasisi za kukopesha pesa na watu binafsi.