Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Mkuranga ampongeza mkurugenzi kwa amani

3f2e95e2b4562d4cad90bf2b62f9e8a0 DC Mkuranga ampongeza mkurugenzi kwa amani

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Mkuranga katika Mkoa wa Pwani, Filberto Sanga, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mshumu Munde na wataalamu wake kufanikisha uchaguzi mkuu uliopita kuwa wa haki hali iliyofanikisha utulivu na amani.

Akifungua kikao cha Baraza la Ushauri Wilaya ya Mkuranga jana, Sanga ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho, alisema wilaya ina mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano wa madiwani, wataalamu na ofisi yake hali iliochangia Mkuranga kuwa wilaya ya mfano kwahuduma za jamii na uwekezaji wa viwanda.

Aliwataka wajumbe kujipanga upya kutatua changamoto katika sekta ya elimu hususani kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyetaka ifikapo Februari 28, mwakani wanafunzi wote wawe darasani huku wakikaa kwenye madawati.

Kuhusu wajasiriamali, Sanga aliwaagiza watendaji kata na vijiji kuhakikisha wafanyabiashara wote wana vitambulisho huku watumishi wakitanguliza kauli nzuri na uadilifu katika matumizi ya fedha za serikali.

Alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mohamedi Mwela, kusimamia mchakato wa uwepo wa Mji Mdogo wa Mkuranga utakaochangia kuwapo kasi ya maendeleo sambamba na utatuzi wa migogoro ya ardhi, wafugaji na wakulima.

Chanzo: habarileo.co.tz