Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Mjema:  Wenye shida njooni hata bila miadi

4c7a3335f84644d6123419cb6641eb89 DC Mjema:  Wenye shida njooni hata bila miadi

Thu, 24 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

"Wananchi! Milango ipo wazi njooni mimi si DC (mkuu wa wilaya) wa appointment (miadi), hapana nitamsikiliza kila mtu kwa wakati wowote na napenda sana kwenda field (eneo husika) ili kujua changamoto za wananchi ni zipi."

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Sophia Mjema, alisema hayo jana katika makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM)-Taifa na Mjema kushika nafasi yake.

Alisema atasikiliza kero za wananchi muda wowote na kwenda katika eneo husika ili kuona hali halisi na kwamba, yeye si kiongozi wa kuwekea miadi ili kuonana naye kusikiliza shidana kuzitafutia ufumbuzi.Aliwaagiza wakuu wa idara na vitengo mbalimbali wilayani humo kutozima simu kwa kuwa tatizo linaweza kutokea muda wowote na linapaswa kutatuliwa kwa wakati.

Alisema kwa kuwa wananchi wana kero nyingi hivyo, lazima simu za wakuu wa idara na vitendo ziwe wazi saa 24 kwani wakati wowote inaweza ikatokea dharura inayohitaji kutatuliwa haraka.

"Wananchi milango ipo wazi njooni mimi si DC wa appointment (miadi), hapana nitamsikiliza kila mtu kwa wakati wowote na napenda kwenda field (eneo husika) sana ili kujua changamoto za wananchi ni zipi,"alisema.

Naye Kihongosi alishukuru watumishi wa ofisi hiyo kwa ushirikiano waliomwonesha katika kipindi chote alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz