Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC: Mifugo ikila miti ya Serikali mtapigwa faini

FEDHA DC: Mifugo ikila miti ya Serikali mtapigwa faini

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Amiri Mkalipa ametoa tahadhari Wafugaji na kuwataka kuwa makini na miti inayopandwa maeneo ya Wilaya hiyo isiliwe na mifugo wanayofuga kwakuwa watakumbana na faini na mifugo kutaifishwa “Tukimkamata Mfugaji anayelisha mbuzi atapigwa faini au tunachukua mbuzi tunapika supu”

Akiongea wakati wa zoezi la upandaji miti Wilayani humo ikiwa ni Maadhimisho ya Sherehe za Muungano ambayo kilele ni kesho Aprili 26, amesema wameweka faini ambazo zimewekwa kwa mujibu wa Kijiji husika au mifugo kutaifishwa kwasababu bila kuweka faini kubwa kila mwaka watakuwa wakirudia kupanda miti maeneo ambayo yalishapandwa miti.

"Ni kweli bila kuweka sheria kali tutakuwa tunarudia maeneo ambayo pengine mwaka jana miti ilipandwa na ikaliwa na mifugo au uangalizi mbovu hatutaki hilo litokee, katika kuadhimisha Muungano mwaka huu Hai tumepanda miti zaidi ya 1000”

"Tunapanda miti na kuitunza, tumeweka sheria kali na tutaijengea ili mbuzi na wanyama wengine wasile, kama unataka mifugo iendelee kuwa salama hakikisha na miti yetu inakuwa vizuri”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live