Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Danstan Kyobya na Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi wamemaliza mgogoro wa Wafugaji na Wakulima uliodumu kwa muda mrefu katika Kata ya Ching'anda na Chita.
Viongozi hao walifika na kusikiliza changamoto zilizokua zikiwakabili wananchi hao ambapo DC, Kyobya alimuelekeza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kilombero kuwashikilia Wafugaji wawili Orandi Makenzi na Richard Maveregachu kwa ajili ya mahojiano baada ya wananchi wengi kulalamika kuwa wamekuwa wakilisha mifugo yao kwenye mashamba ya Watu.
Kwa upande wake Mbunge Kunambi amemshukuru DC Kyobya kwa kufika katika kata hiyo na kutatua mgogoro huo huku akitumia mkutano huo kueleza mambo makubwa ambayo Rais Dkt Samia ameyafanya katika Jimbo la Mlimba kwenye sekta za elimu, afya na miundombinu.