Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Mboneko aagiza Jeshi kuwashughulikia machangudoa Shinyanga

Dc Mboneko Ldsd.jpeg DC Mboneko

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amelitaka jeshi la jadi maarufu Sungusungu katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kuhakikisha linaondoa wale wote wanaofanya biashara ya kuuza miili katika maeneo ya vijijini.

DC Mboneko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa jeshi hilo pamoja na sungusungu wote, ambapo amesema watu hao maarufu kama ‘nzige’ hutumia kipindi cha mavuno kwenda kuwalaghai wanaume kwenye vijiji hivyo.

"Ninaagiza muwaondoe mara moja, wanakuja hapa na kreti la bia na na soda wanaondoka na magunia ya mpunga, wanaondoka na ndoo ya pesa. Wanapanga foleni na nyie mnawashughulikia tu bila hata kuwapima, mtapata maradhi bure.

"Asubuhi mpaka asubuhi mnapanga foleni kuwashughulikia, nyie mnaita kuchemsha hamjawathibitisha, hata kwa daktari, naagiza muwafukuze, wanatuharibia watoto. Wanaleta magonjwa," amesema DC Mboneko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live