Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Mbeya atembelea nyumba ya mgombea inayodaiwa kutaka kuchomwa moto

17675 Pic+nyumba TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika akiongozana na  kamati ya ulinzi na usalama amefika nyumbani kwa mgombea udiwani wa CCM kata ya Nsalaga, Mchungaji David Ngogo huku kukiwa na habari kwamba nyumba ya mchungaji huyo inataka kuchoma moto.

Vitu vilivyokutwa jirani na nyumba hiyo ni madumu ya mafuta ya petroli.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili Septemba 16, 2018 huku Ntinika akikwepa kuzungumzia kwa kina akieleza kuwa anasubiri taarifa sahihi za tukio hilo.

“Kwa sasa ninazunguka katika kata zinazofanya uchaguzi siwezi kuzungumza chochote sasa hivi nipo kuzunguka kwenye kata zinazofanya uchaguzi, sitoweza kuzungumza chochote kwa muda huu mpaka nikimaliza ziara,” amesema.

“Bado vyombo vyetu vinaendelea kuchunguza tukio hili, naomba unitafute kuanzia saa nane mchana.”

Hata hivyo, kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema hana taarifa za tukio hilo, “ngoja nifuatilie kwanza nitakupa jibu.”

Wakizungumza na MCL Digital mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea alfajiri ya kuamkia leo.

Chanzo: mwananchi.co.tz