Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Mbeya aiomba TCRA kuharakisha mchakato wa sheria wizi mtandaoni

Tcra Pic Data DC Mbeya aiomba TCRA kuharakisha mchakato wa sheria wizi mtandaoni

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua ameiomba Mamlaka ya Masiliano Tanzania (TCRA) kuharakisha mchakato wa sheria za wizi mtandaoni kutokana na kukithiri kwa wimbi hilo nchini.

Dk Chuachua ametoa ombi hilo leo Jumatano Novemba 17, 2021 wakati akifunga mafunzo ya umoja wa mafundi simu 95 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yaliyoratibiwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na TCRA.

Amesema kuwa kumeibuka kwa changamoto ya wizi mtandaoni hivyo wakati mchakato huo ukiendelea mafundi simu wapatiwe elimu ya kukabiliana nayo kutokana na mchango mkubwa kwa Serikali kuibua matukio ya kiharifu.

''Ili kuweza kuliweKa Taifa kuwa salama ni vyema mchakato wa sheria ya kuthibiti wizi mtandaoni ikaharakishwa pamoja na mafundi simu kuisaidia Serikali kuwafichua kwani wamekuwa wakipokea simu kutoka kwa wateja mikoa na maeneo mbalimbali'' amesema.

Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Asajile John amesema lengo la kutoa mafunzo kwa mafundi simu na kuwapatia leseni ni kuweza kuthibiti matukio ya wizi mtandaoni.

''Mafundi simu mliopata elimu hii tunaomba mkawe chachu ya kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na wizi mtandaoni kwani mmekuwa msaada mkubwa sana kwa Jeshi la Polisi kuibua wahalifu na kufanikisha kukabiliaba na matukio ya kihalifu''amesema.

Amesema kutokana na ushirkiano mkubwa wanaotoa kwa vyombo vya dola ndio umepekelekea TCRA kwa kushirikiana na DIT kutoa mafunzo ya ngazi tofauti ili kuboresha taaluma yao kwa kujiajiri na kujiongezea kipato.

''Tunaomba Serikali kuwapatia mikopo mafundi simu ambao wamepata mafunzo na kuwa na leseni ili kuwawezesha kuboresha taaluma zao na kuwa na mchango mkubwa kwa Serikali.''amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Preksedis Ndomba ameomba wadau kushirikiana kuwawezesha mafundi simu kupata mafunzo ili kuwajengea uwezo wa kutambulika na kuthibiti mafundi simu wasio rasmi.

Amesema kuwa DIT wanaendelea kutanua wigo wa kuendeleza sekta ya teknolojia ya ujenzi na madini ili kuleta chachu katika katika kufikia azma ya Serikali ya uchumi wa viwanda.

Fundi simu mwanamke kutoka Wilaya ya Mbeya, Upendo Lunda amesema kuwa elimu waliyoipata itakuwa chachu katika kuboresha teknolojia rahisi ya matengenezo ya simu na kutoa ajira kwa vijana.

Chanzo: mwananchidigital