Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC: Matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro Liwale

D192E170 E51F 4701 989B 154A1B944DB6.jpeg DC: Matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro Liwale

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Liwale mkaoni Lindi, yaja na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji sita wilaya humo, jambo ambalo litasaidia kulinda ikolojia, na hivyo kuwafanya tembo kutohama katika makazi yao.

Vijiji hivyo sita ni pamoja na Ndunyungu, Mpengere, Ngorongopa, Mitawa, Lubaba na Nambinda; ambako kumekuwa na ya uharibifu ikolojia, na hivyo kuwafanya tembo kuingia katika makazi ya binadamu.

Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Goodluck Mlinga, amesema kuna maeneo ambayo njia za tembo zimeharibiwa, jambo ambalo linasababisha wanyama hao kuingia katika mashamba ya watu.

“Tuna vijiji 76 katika wilaya hii, kati hivyo, vijiji 64 vimevamiwa na tembo, vijiji 12 ndiyo bado hvijavamiwa. Kulima kwenye kwenye njia za tembo, kunaharibu ikolojia na kusababisha wanyama hao kuingia kwenye makazi ya watu,” amesema na kuongeza;

“Hivyo kama mchakato huu utakamilika, utasaidia kumaliza tofauti na migogoro baina ya hifadhi na vijiji au vijiji kwa vijiji, pia utaongeza thamani ya ardhi.” Mpamgo huo unafanywa kwa ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Hifadhi ya Nyerere, Frankfurt Zoological Socierty, Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) na ofisi ya Kamisha Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Lindi. Wananchi katika vijiji hivyo, wamepongeza juu ya mradi huo, wakiamini kuwa licha ya kumaliza migogoro ya kimpaka iliyopo, lakini pia watapata hatimiliki ambazo zitawasaidia kupata mikopo na hivyo kujiendeleza kiuchumi. "Naishukuru tume kuja kutupatia elimu ambayo itatusaidia kuwa na matumizi mazuri ya ardhi na hivyo kutuondolea migogoro. Familia zetu pia zitanufaika kwani tumeambiwa hati miliki za ardhi zitalewa,” amesema Tabia Matala, mjumbe wa kamati ya Usimamizi wa Ardhi, Kijiji cha Ndunyungu. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Makata, Mpungu Mfaume, amesema anashukuru mradi huo kwa kufika Liwale kwani kumekuwa na changamoto nyingi za ardhi. "Mwanzo hatukuwa tunafahamu utaratibu mzuri wa matumizi ya ardhi, kwa kupata elimu hii itatusaidia kupanga matumizi bora na kuondoa migogoro, tunaishukuru Serikali kwa kutuletea mpango huu," amesema Juma Said, Kaimu Mwenyekiti Kijiji cha Lubaba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live