Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Matinyi awataka kutafuta fursa za ajira

Malinyi Nyi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi, amewataka vijana wilayani humo kujikwamua na tatizo la ajira kwa kutumia fursa nyingi za mikopo zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita.

Matinyi ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo mapema mwezi huu akichukua nafasi iliyoachwa na Mwanahamisi Munkunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Akitoa salamu zake katika semina ya uongozi na itifaki ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani hapo leo Julai 8, Matinyi amesema vijana wanastahili kudumisha amani na kuweka bidii katika shughuli za kiuchumi ili kuitikia mwito wa serikali wa kupunguza tatizo la ajira nchini.

Amesema fursa za mikopo zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zinawalenga zaidi vijana ambao ni nguzo muhimu ya uchumi katika taifa letu.

Ametoa mwito kwa vijana wanaotaka kuzijua fursa hizo kufika katika ofisi za wilaya ili waelimishwe.

Naye mgeni rasmi aliyeifunga semina hiyo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Ramadhani Mlao, alisisitizia umuhimu wa viongozi wa UVCCM kujenga mahusiano mazuri miongoni mwao ili waunganishe nguvu za kutetea mazuri yote ya utekelezaji wa ilani ya CCM yanayofanywa na Rais Samia.

Chanzo: Mwananchi