Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Makete akanusha kuhusu baridi kali na barafu

Baridi Kalii Pic Data DC Makete akanusha kuhusu baridi kali na barafu

Fri, 15 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mkoani Njombe, Juma Sweda amekanusha kuhusu video fupi zilizosambaa mitandaoni zikionesha uwepo wa baridi kali na barafu ndani ya Wilaya hiyo.

Sweda amesema kuwa ni kweli mazingira ya Wilaya ya Makete yana hali ya hewa ya baridi lakini Watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakipotosha kwa kusambaza video za maeneo mengine au za muda mrefu na kuzihusisha na wilaya hiyo.

“Makete ina mwinuko mkubwa kidogo ukilinganisha na maeneo mengine na sisi Wilaya yetu mara zote ni baridi lakini inavyoonyeshwa kuna barafu na Watoto wanatembea kwenye barafu sio sahihi na eneo lile halipo Makete kwahiyo hatuna zile changamoto za barafu mpaka zinadondoka barabarani”amesema Juma Sweda

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema hali ya hewa ya baridi iliyopo kwa sasa katika baadhi ya maeneo mkoani humo ni fursa kwa Watanzania kufanya utalii wa baridi kwa kuwa imekuwa ni moja ya kivutio hususani katika hifadhi ya Kitulo iliyopo wilayani Makete.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live