Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Ludewa aapa kula sahani moja na maafisa Ugani

DC Ludewa Aapa Kula Sahani Moja Na Maafisa Ugani DC Ludewa aapa kula sahani moja na maafisa Ugani

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuhakikisha kuwa maafisa ugani wanafanya kazi yao ipasavyo na kuwafikia wakulima mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amesema anahitaji kupitia ripoti za utendaji kazi za maafisa hao ili kujiridhisha kwa kile kinachotendeka.

Mwanziva ameyasema hayo katika mkutano wa wadau wa kilimo ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo uliolenga kuimarisha sekta ya kilimo wilayani ya Ludewa.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Sunday Deogratius amesema wilaya hiyo bado ina akiba ya maeneo ya kilimo ambayo yanahitaji wawekezaji huku afisa kilimo wa wilaya hiyo Godfrey Mlelwa akitaja kiwango cha maeneo yaliyolimwa na yasiyolimwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live