Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Kusini Unguja asema amempa saa 48 mfanyabiashara kuondoka ili kumlinda

66038 DC+PIC

Mon, 8 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa amesema uamuzi wa kumpa saa 48, Salome John kuondoka katika wilaya hiyo ulilenga kumlinda.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 8, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Kitwana alichukua uamuzi huo juzi kwa madai kuwa mwanamke huyo huwatumikisha kingono wasichana alioahidi kuwapa kazi ya kuuza baa. Wasichana  hao tayari wamerejeshwa Tanzania Bara baada ya kumlalamikia mwajiri wao huyo.

Amesema mfanyabiashara huyo amekuwa akilalamikiwa na wakazi wa shehia ya Kizimkazi kwa kutoridhishwa na matendo yake, ikiwa ni pamoja na kuwaingiza katika mgogoro wanandoa mbalimbali.

Amesema Salome bado anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

Chanzo: mwananchi.co.tz