Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Korogwe apiga marufuku watu kuoga mto Ruvu

17960 New+Document+%25281%2529 TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Korogwe: Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Kissa Kasongwa amewapiga marufuku wananchi kuacha kuoga ndani ya mto Ruvu kwa sababu wanaharibu mazingira pamoja na kuhatarisha magonjwa ya milipuko.

Alitoa amri hiyo  wakati wa maadhimisho ya siku ya usafi duniani yaliyofanyika kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali fukwe za mto Pangani mjini Korogwe.

Alisema tabia ya kuoga mtoni mbali ya kuondoa hadhi na utu pia kuhatarisha magonjwa ya milipuko na kuharibu mazingira.

"Mwanaume ama mwanamke, tena mtu mzima, kinamshushia hadhi yake anapoonekana mbele za watu anaoga mtoni...huku ni kuuchafua Mto Pangani ambao maji yake yanakwenda sehemu kubwa" alisema Kissa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema anataka Korogwe iwe mfano wa kuigwa katika suala zima la usafi na utunzaji wa mazingira kwa sababu ipo eneo ambalo wasafiri kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani hupitia.

Naye Ofisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji Korogwe Abdallah Lungo, alisema mbali ya kuoga lakini pia tabia ya kutupa takataka kando au ndani ya mto ni vyema iachwe kwa sababu ni uharibifu wa mazingira pamoja na kuyachafua maji.

Alisema kwa sasa mji wa Korogwe umekuwa safi na siri kubwa ni kutokana na ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwamo asasi ya Nipe Fagio kuwaunga mkono .

Katika maadhimisho hayo, jumla ya  wananchi 650 walishiriki shughuli za usafi kwakusafisha maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji Korogwe ikiwemo soko la zamani la Old Korogwe, Msambiazi, Daraja la Mbeza na Shule ya Sekondari ya old korogwe.

Chanzo: mwananchi.co.tz