Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Kinondoni acharuka ubakaji kwenye 'school bus'

WhatsApp Image 2022 09 07 At 5.52.30 PM.jpeg DC Kinondoni acharuka ubakaji kwenye 'school bus'

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: EATV

Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa kuweka Matron katika gari za kubeba wanafunzi baada ya kuibuka kwa vitendo vya ubakaji kwa watoto vinavyodaiwa kufanywa na madereva.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe amesema kwamba amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na walezi, wakidai watoto wao kufanyiwa vitendo vya ubakaji katika magari ya shule na kwamba vinasababishwa na madereva wa magari hayo wasiowaadilifu.

Akizungumza jana Septemba 07 katika Mkutano wa Maofisa Ustawi wa Jamii nchini akiwa Jijini Dar es Salaam, Gondwe amewataka wazazi na walezi kuwa makini kufuatilia taarifa za watoto na kujenga ukaribu, ilikusudi wanapotendewa au kuona viashiria vya vitendo hivyo waweze kutoa taarifa.

“School Bus mtoto anapanda wa kwanza anashuka wa mwisho na bahati mbaya wazazi hawafuatilii  nyendo za watoto, hivi karibuni kuna mama alikuja kulalamika mwanaye alifanyiwa ukatili. Dereva alipaki gari akaenda kumfanyia mtoto shambulio la kikatili na mtoto alivyofika nyumbani alikuwa huru kuzungumza na mama” Godwin Gondwe, DC Kinondoni.  

Chanzo: EATV