Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Kilolo apiga marufuku unywaji pombe kijamaa

100555 Dc+pic DC Kilolo apiga marufuku unywaji pombe kijamaa

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya (DC) ya Kilolo Mkoa wa Iringa nchini Tanzania, Asia Abdallah amepiga marufuku mtindo wa kunywa pombe kwa kupokezana ndani ya chombo kimoja ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (Codiv-19).

Kwa asili wakazi wa Iringa hutumia chombo kimoja kunywa pombe inayotengenezwa kwa mahindi   ‘komoni’  kwa kupokezana kama watakuwa zaidi ya kumi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Machi 28, 2020, Asia amesema mbali na ugonjwa wa corona, unywaji wa pombe kijamaa unawaweka kwenye hatari ya kupata magonjwa mengine ya mlipuko.

“Kama walizoea kunywa pombe kwa kupokezana kwamba huyu anapuliza anakunywa, anampa mwingine anapuliza anakunywa hapana, hii haitakiwi kabisa, wanunue pombe wakanywe nyumbani na kila mtu atumie chombo chake,” amesema Asia.

Amesema katika kipindi cha siku 30, hakuna mikusanyiko inayoruhusiwa ndani ya wilaya hiyo.

“Hata vilabuni haturuhusu watu, hatuwezi kuzuia wasinywe pombe lakini wakanywe nyumbani kwao,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Pia Soma

Advertisement
Kwa upande wake, mzee Erick Kalinga amesema unywaji wa pombe kijamaa ni ishara ya upendo kwa wanywaji japo mtindo huo wanapaswa kuachwa kutokana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali.

“Hata kama huna hela unaweza kwenda kilabuni kwa sababu mmoja akinunua wengine mtakunywa tu, huwa tunakunywa hivi kuonyeshana upendo na umoja lakini tumesikia wito wa Serikali lazima tuachane na hili,” amesema Kalinga.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz