Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Kigoma: Wananchi wamenituma nikubusu Rais Samia

Ester Mahawe Ester Mahawe

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ester Mahawe ameamua kuibusu picha ya Rais Samia baada ya hitimisho la ziara yake ya siku tatu Mkoani Kigoma ambapo amesema Watu wa Kigoma wamemtuma kumbusu Rais kama ishara ya upendo kwake na kuthamini mazuri aliyowafanyia Kigoma.

DC Ester amesema ameamua kuibusu picha ya Rais na kuikumbatia kwasababu ya mazuri anayoyafanya hususani katika Mkoa wa Kigoma kwa kupeleka miradi ya kimaendeleo ikiwemo Afya, Elimu, Barabara na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuifungua Kigoma katika Sekta hizo muhimu.

DC Ester ameshukuru Rais Samia kwa Wilaya yake ya Kigoma kupokea kiasi cha Tsh. Bilion 31.6 tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

"Mama Samia umetuheshimisha sana, Sisi Wanao wa Kigoma, hakika busu hili wamenituma likufikie kwa niaba yao wote Kwa mema mengi uliyotufanyia na uliyoahidi kuyafanya, hakika Kigoma tunakupenda sana"

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan imemalizika Mkoani Kigoma kwa kuongea na Wananchi wa Mkoa huo katika Viwanja vya Lake Tanganyika huku awali akitembelea Wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu na Buhigwe na kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika jitahada za kuboresha Mkoa huo na kuongeza fursa za kiuchumi na kibiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live