Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mh. Jokate Mwegelo amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za TANESCO wilayani humo na kukutana na malalamiko lukuki kutoka kwa Wananchi waliofika katika ofisi hizo, wakidai kucheleweshwa kwa uwekwaji umeme majumbani mwao, ikiwemo kero ya kukatika kwa umeme na hivyo kusababisha hasara kubwa kila uchwao kwa vyombo vinavyotumia nishati hiyo.
Mh. Jokate ameagiza kuswekwa rumande kwa baadhi ya watendaji wa idara hiyo, huku akiutaka uongozi kuhakikisha inatatua kero inayowakabili wananchi haraka iwezekanavyo.
‘Kuna watandaji wahusika wa control number, quantity surveyors na waandikisha mita waliwekwa ndani kuhojiwa, Ila nilitaka uongozi mzima wakiongozwa na meneja wa Tanesco Kisarawe kuhakikisha wananchi wote waliopo ofisi wanatatuliwa kero zao na wakeshe mpaka wananchi wote waishe. Ila Pia uongozi wa pale inafaa ubadilishwe maana usimamizi ni mbovu na hakuna huduma bora kwa wananchi’- DC Jokate Mwegelo